Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona wamsajili Raphinha

 Barcelona wamsajili Raphinha


Barcelona wametangaza kuwa wafikia makubaliano kumsajili winga wa Brazil Raphinha kutoka Leeds United, akisubiri kufanyiwa vipimo vya afya.

Taarifa rasmi kwenye tovuti ya klabu hiyo kuhusiana na hatua hiyo inasema: "FC Barcelona na Klabu ya Soka ya Leeds United wamefikia makubaliano kuhusu uhamisho wa Raphael Dias Belloli, Raphinha, huku mchezaji huyo akisubiri kufaulu vipimo vya Afya."

Akizungumza mapema leo, meneja wa Leeds alimshukuru Raphinha kwa uchezaji wake, haswa mwishoni mwa msimu wa 2021/22:

"Ingawa ni ngumu sana kumpoteza Raphinha nitasema haya kuhusu yeye - ikiwa unafikiria kuhusu kijana, ambaye alikuwa na uhakika wa kupunguzwa kwa ada ya uhamisho kwa asilimia 100 kwenda Barcelona ikiwa tutashuka daraja na kisha uangalie alivyo cheza na kujitolea kuhakikisha klabu inasalia Ligi kuu.

"Nadhani itakuwa ngumu kwa mtu yeyote, wa miaka 23, 24 mwenye uwezo wa aina yake na nafasi aliyo ipata kuacha kwenda kufanya kazi."

Post a Comment

0 Comments