Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea kumsajili Nathan Ake wa Man City

Chelsea wanakaribia kumsajili Mlinzi Nathan Ake kutoka Manchester City, Wakiendelea na juhudi zao za kuimarisha safu yao ya Ulinzi baada ya wacheziji wao kadhaa wa safu ua Ulinzi kuondoka.

The Blues wanahitaji vijana ambao ni damu changa ili kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya kuondoka kwa Antonio Rudiger na Andreas Christensen baada ya kumalizika kwa mikataba yao.


Chelsea pia wamefanya mazungumzo Napoli juu ya Uhamisho wa beki wao wa kati Kalidou Koulibaly, na ikiwa Uhamisho huo utafanikiwa basi anaweza kuungana na Nathan Ake Stamford Bridge.

Vyanzo vya habari vimeripoti kwamba ada ya pauni milioni 45 imekubaliwa na Man City kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, ingawa mkataba huo na hela za nyongeza bado hazijakamilika.

Ake ambae ni mchezaji wa zamani wa Chelsea,  anatamani kurejea katika klabu hiyo na hivyo haitarajiwi kama maslahi binafsi yatakuwa kikwazo. Uwezo wake wa kucheza namba tofauti uwanjani unaonekana kumvutia kocha mkuu Thomas Tuchel, na mchezaji huyo anaweza kuhudumu kama beki wa kati, beki wa kushoto na winga wa kushoto.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27 amekaa miaka mitano na Chelsea kabla ya kusajiliwa na klabu yake ya zamani ya Bournemouth kwa mkopo mwaka 2017.

Ake alijiunga na City kutoka Cherries kwa £41m msimu wa majira ya joto mwaka 2020 na ametumika kama mchezaji wa kikosi cha kwanza, akianza mechi tisa za Premier League katika msimu wake wa kwanza na kumi msimu uliopita - ingawa alishinda mataji mfululizo ya ligi. .

Licha ya Ake na Koulibaly, Chelsea pia wanavutiwa na mabeki wengine wa kati kama Presnel Kimpembe na Mlengwa wa muda mrefu Jules Kounde. Aliyepewa kipaumbele ni Matthijs de Ligt ambae anaonekana yuko mbioni kujiunga na Bayern Munich.

Post a Comment

0 Comments