Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona 'Wagoma' Kuongeza Ofa Kwa Robert Lewandowski

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Barcelona 'Wagoma' Kuongeza Ofa Kwa Robert Lewandowski RAIS Wa Klabu Ya Barcelona Joan Laporta Amethibitisha Kwamba Klabu Hiyo Haina Mpango Wa Kuongeza Ada Ya Usajili Kwa Mshambuliaji Wa Bayern Munich Robert Lewandowski.

Lewandowski Anahitaji Kuondoka Na Kujiunga Barcelona Kabla Bayern Munich Hawajaanza Maandalizi Ya Msimu Mpya July 12, Lakini Vilabu Hivyo Vimeshindwa Kufika Muafaka Juu Ya Uhamisho Wa Mchezaji Huyo, Huku Klabu Inayomuhitaji Ya Barcelona Mara Ya Mwisho Ilituma Kiasi Cha Euro Milioni 40 Ambapo Kiasi Hicho Ni Kidogo Kulinganisha Na Kiasi Anacho Uzwa Mchezaji Huyo.

Bayern Hawapo Tayari Kupokea Ofa Chini Ya Euro Milioni 50-60 Kwajili Ya Uhamisho Wa Robert Lewandowski. Rais Wa Barcelona Laporta Akihojiwa Na Waandishi Wa Habari Kama Kunauwezekano Wa  Mshambuliaji Wa Bayern Munich Robert Lewandowski Kujiunga Nao Alisema Kwamba Hayupo Tayari Kuongeza Kiasi Cha Fedha Zaidi Ya Euro Milioni 40.

Pini Zahavi Wakala Wa Masuala Ya Usajili Wa Lewandowski Amekuwa Akishirikiana Na Barcelona Kuona Kama Kunauwezekano Wa Kuwashawishi Bayern Munich Kupunguza Ada Hiyo Ya Uhamisho Ili Mteja Wake Aweze Kujiunga Na Miamba Hiyo Ya Uhispania Lakini Mbaka Sasa Imeshindikana Kuwashawishi Bayern Kushusha Dau Hilo.

Post a Comment

0 Comments