Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester United Wamuhitaji Lisandro Martinez wa Ajax

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Manchester United Watuma Ofa Ajax Kwajili ya Mlinzi Lisandro Martinez

Manchester United wametuma ofa ya euro milioni 45 kwa mabigwa wa ligi kuu ya Uholanzi Ajax kwajili ya beki Lisandro Martinez.

United wamehamishia nguvu zao kwa mlinzi huyo raia wa Argentina baada ya kuwa katika hatua nzuri kuzinasa saini za wachezaji Frenkie de Jong kutoka Barcelona na Tyrell Malacia kutoka Feyenoord ya Uholanzi.

Kwa sasa Manchester United imeweka kipaumbele kwa Martinez baada ya kocha wa United Erik ten Hag kuhitaji huduma ya beki huyo mwenye miaka 24 Old Trafford licha ya kuwa na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya vilabu vinavyo shiriki Ligi kuu nchini Uingereza ikiwemo Arsenal Ambayo nayo inahitaji huduma ya beki huyo.

Manchester United wamepeleka ofa kubwa kuliko ofa mbili zilizo pelekwa na Arsenal Ambao nao wanamuhitaji beki huyo kwa euro milioni 40.

Ajax wapo tayari kumwachia Martinez kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 50, lakini United wanamatumaini kuwa kwa ofa waliyo peleka uhamisho huo utafanikiwa huku wakiamini mchezaji huyo yupo tayari kuja Old Trafford.

Lisandro Martinez anamudu kucheza nafasi mbalimbali, anauwezo wa kucheza kama beki wa kati, beki wa kushoto, na pia anauwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji.

United Wanaamini Watakamilisha Sajili Kwa Baadhi ya Wachezaji Mapema Kabla ya Kuondoka na Kwenda Kujiandaa na Msimu Mpya nchini Thailand na Australia Siku Ya Ijumaa. Usajili wa Tyrell Malacia umeshakamilika, wakati huo United wanaimani mbaka kufika ijumaa usajili wa kiungo De Jong kutoka Barcelona utakuwa nao umekamilika.


 

Post a Comment

0 Comments