Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Ronaldo Aomba Kuondoka Man United
Cristiano Ronaldo ameomba kuondoka Manchester United kabla dirisha la usajili halijafungwa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza haujaanza.
Ronaldo mwenye miaka 37 amasekumwa kufanya maamuzi hayo akiwa na lengo la kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ronaldo amaefanikiwa kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa misimu 19 mfululizo na sasa anaona ndoto yake kuendelea kushiriki michuano hiyo haiwezi kutimia kama ataendelea kusalia Manchester. Ronaldo anashikilia rekodi ya kutwaa taji hilo mara tano akicheza michezo 183 na kufanikiwa kufunga magoli 140 na kuchangia pasi za magoli 42.
Ronaldo anaamini ana miaka mitatu kama sio minne ya yeye kucheza soka la ushindani kabla haja staafu hivyo anahitaji kutumia muda wake ulio bakia kucheza katika timu itakayo kuwa na uwezo wa kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya mara kwa mara.
Klabu zilizo onyesha nia ya kumuhitaji Ronaldo katika siku za hivi karibuni ni pamoja na Chelsea, Bayern Munich,Paris Saint-Germain na Sporting CP Ambazo zote zina nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.
Ronaldo ambaye amabakiza mwaka mmoja katika mkataba wake ameiomba United imuuze kama kuna timu inayo shiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao italeta ofa nzuri.
0 Comments