Ticker

6/recent/ticker-posts

Bayern Munich: Bila pauni milioni 60 Robert Lewandowski Hauzwi.

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BAYERN Munich wasisitiza bila pauni milioni 60, Robert Lewandowski Hauzwi.

Mapema wiki hii, klabu ya FC Barcelona kutoka Uhispania imepeleka ofa ya pauni milioni 34.4, lakini Bayern wamesisitiza mshambuliaji huyo hauzwi, ingawa amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake.

Mwezi uliopita, Sky Germany iliripoti mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliiambia Bayern hataongeza mkataba wake hadi mwisho wa msimu wa 2022/23.

Lewandowski ameiambia klabu hiyo ya Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, anataka kupata changamoto mpya. Sky iliongeza Lewandowski angependa kuhamia Barcelona msimu huu wa joto badala ya kusubiri kuwa mchezaji huru. 

Oliver Kahn, Mtendaji Mkuu wa Bayern Munich, aliiambia Amazon Prime, Aprili mwaka huu kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland hataondoka Allianz Arena msimu huu wa joto. 

"Tutakuwa wajinga kumuuza mchezaji ambaye anafunga mabao 30 hadi 40 kwa msimu," alisema Khan mlinda mlango wa zamani wa Bayern na Ujerumani. "Ana mkataba hadi Juni 2023 na bila shaka tutakuwa naye kwa msimu mwingine." 

Lewandowski amekuwa na mabingwa hao wa Ujerumani tangu mwaka 2014 na amefunga mabao 344 katika michuano yote na kuisaidia Bayern Munich kushinda mataji manane ya Bundesliga katika misimu minane iliyopita, pamoja na mataji matatu ya Ujerumani, na ametawazwa mfungaji bora wa ligi hiyo kwa msimu wa tano mfululizo. 

Lewandowski ametumia muda mwingi wa uchezaji wake nchini Ujerumani baada ya kujiunga na Borussia Dortmund kutoka Lech Poznan mwaka 2010.

 Kwa mujibu wa FC Barcelona wanavutiwa sana na Lewandowski. Xavi anataka sana mshambuliaji wa kiwango cha kimataifa ambaye anaweza kufikikisha mabao 30 au zaidi kwa msimu. Mkataba wa miaka miwili au mitatu unakaribia kukamilika na mshahara wa kati ya pauni milioni 30 hadi 34 kwa mwaka.

Post a Comment

0 Comments