Ticker

6/recent/ticker-posts

Pape Sakho kuendelea kuitumikia Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Pape Sakho kuendelea kuitumikia Simba
KLABU ya Simba imesema kwa sasa haina ofa kutoka kwa timu yoyote ikieleza inamhitaji kiungo mshambuliaji wake, Pape Sakho, baada ya ofa ya awali kutoka Al Hilal ya Sudan kushindikana. 

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, akihojiwa amesema kwamba ofa kutoka Al Hilal ya Sudan ilikuwa nzuri, lakini muda walioiwasilisha wakati huo haukuwa rafiki kumuuza mchezaji huyo raia wa Senegal. "Kwa sasa hakuna ofa yoyote iliyokuja kumtaka Sakho, tuliweka wazi huko nyuma kuwa ilikuja ofa kutoka Sudan na ilikuwa nzuri tu, lakini muda haukuwa rafiki kufanya hiyo biashara, ikashindikana," alisema Ahmed. 

Aliongeza falsafa ya Simba miaka yote ni pamoja na kucheza soka na kununua wachezaji, lakini inafanya biashara ya mpira ambayo ni kuuza wachezaji na kutafuta wengine mbadala wake. 

"Mchezaji mzuri lazima azungumzwe kuuzwa, huwezi kuwa na wachezaji kama umewazaa wewe, wala hawahusishwi na timu yoyote, lakini Sakho anatajwa huku na huko kwa sababu ya kiwango chake na sisi tunafurahi kuona wachezaji wetu wanahusishwa na klabu mbalimbali Afrika, hata sasa ikija ofa nzuri tutaiangalia, kwa sasa bado yupo sana Simba," Ahmed alisema.

Kiungo huyo mshambuliaji alisajiliwa Simba akitokea Teungueth ya Senegal na licha ya timu kutokuwa na msimu mzuri, nyota huyo amekuwa msaada mkubwa kwa kuiwezesha kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Post a Comment

0 Comments