Ticker

6/recent/ticker-posts

Klabu ya Chelsea Kumuuza Hakim Ziyech Kwa Pauni 33.3M

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Chelsea, imefikia maamuzi ya kumuuza winga wa timu hiyo, Hakim Ziyech ambaye alitua kikosini hapo mwaka 2020 kwa pauni 33.3m.

Winga huyo alifanya vizuri wakati akiwa Ajax ambako alidumu kwa misimu minne, akifunga mabao 49 akicheza mechi 165, huku akishinda taji la Ligi ya Uholanzi chini ya Kocha Erik ten Hag.

Kocha Thomas Tuchel na mmiliki mpya wa klabu hiyo, Todd Boehly, wamekubaliana kumuuza winga huyo ambaye kwa sasa anatajwa kuwindwa na AC Milan.

Ziyech ndani ya Chelsea alishindwa kupata nafasi ya moja kwa moja na msimu uliopita akianza mara 14 katika mechi 38 za Premier, huku akishindwa kucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati Chelsea ikiwaza kumuuza winga huyo, mpango wao ni kumvuta Ousmane Dembele wa Barcelona na Raheem Sterling wa Man City.

Ziyech atakuwa ni mchezaji mwingine ambaye anaondoka kikosi hapo baada ya Antonio Rudiger na Andreas Christensen, huku Romelu Lukaku akitolewa kwa mkopo kwenda Inter.

Post a Comment

0 Comments