Ticker

6/recent/ticker-posts

Kibu Denis kuwakosa Vipers Ligi Ya Mabingwa Afrika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MSHAMBULIAJI wa Simba, Kibu Denis atakosekana ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa muda wa wiki mbili kufuatia kuumia goti kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers ya Uganda.

Katika mchezo huo uliopigwa wikiendi iliopita nchini Uganda na  Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi 1-0  kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajia kupigwa Machi 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Meneja wa mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amefichua kuwa wanatarajia kumkosa mshambuliaji huyo kwa kipindi cha wiki mbili kutokana na kuumia goti kwenye mchezo uliopita dhidi ya Vipers ya Uganda.

“Kibu tutamkosa kwa kipindi cha wiki mbili kutokana na shida ya kuumia goti katika mchezo uliopita dhidi ya Vipers, lakini wachezaji waliobakia sehemu kubwa wapo vizuri na maandalizi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa ambao tutacheza hapa Dar es Salaam.

“Nadhani baada ya wiki mbili kuisha kila kitu kitakuwa sawa na atarejea kwenye majukumu yake lakini kwa sasa malengo na mipango yetu ipo kwenye mchezo wetu ujao ambao tunataka kuona tunaweza kuona ushindi unapatikana ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele,” alisema Ally.


Post a Comment

0 Comments