Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi Ategua Mitego Ya Real Bamako

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kuelekea mchezo wa marudiano hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameshawajua wachezaji hatari wa kuchungwa tutakaporudiana dhidi ya Real Bamako ya nchini Mali.

Timu hizo zitavaana Jumatano ijayo (March,8) usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mchezo wa kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huko Mali huku bao la Yanga likifungwa na Mkongomani Fiston Mayele.

Mabosi kutoka Benchi la Ufundi la Yanga wamewaangalia wapinzani wao katika mchezo wa awali waliocheza ugenini Mali na kuwagundua wachezaji wawili wa kuchungwa watakaporudiana.

Bosi huyo aliwataja viungo wawili washambuliaji wanaotokea pembeni ambao wote raia wa Mali ni Cheickna Diakite mwenye umri wa miaka 18 na Ousmane Kamissoko, 24, wenye spidi, kontroo na uwezo mkubwa wa kukokota mpira.

Aliongeza kuwa wachezaji wengine waliobaki wana uwezo wa kawaida hasa mabeki wao wenyewe hawana spidi hivyo wakiwatumia mawinga na washambuliaji kwa kucheza mipira mirefu basi watapata ushindi katika mchezo wa marudiano.

“Kocha Nabi tayari ameshawajua wachezaji hatari wa kuchungwa tutakaporudiana dhidi ya Real Bamako katika mchezo ambao ni wawili pekee nao ni Kamissoko na Diakite.

“Hao wote ni viungo wanaotokea pembeni, hivyo kocha Nabi amewaona na kuwandaalia mikakati mizito ya jinsi ya kuwazuia ili wasilete madhala golini kwetu tutakaporudiana nao.

“Mabeki wa pembeni wamepewa jukumu hilo la kuhakikisha wanapunguza presha golini kwetu kwa kuwazuia viungo hao wenye uwezo mkubwa wa kukokota mpira huku wakipiga chenga,” alisema bosi huyo.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Cedric Kaze alizungumzia hilo kwa kusema: “Tumeuona ubora wa Bamako katika mchezo uliopita tuliocheza nyumbani kwao Mali.

“Kiubwa tulichogundua ni wazuri katika safu ya ushambuliaji, wapo baadhi ya kuchungwa lakini kwa upande wa mabeki wao ni wazito na hawana kasi, nyumbani kwao tulishindwa kufanya mashambulizi mara nyingi kutokana udogo wa uwanja wao.

“Ninaamini tutakaporudiana hapa kwenye Uwanja wa Mkapa, tutacheza kwa kuutanua uwanja kutokana na ukubwa uliokuwepo na kupata idadi kubwa ya mabao.”

Kibu Denis kuwakosa Vipers Ligi Ya Mabingwa Afrika

MATOKEO YAO CAF 2022/23

Monastir 2-0 Yanga

Yanga  3-1 TP Mazembe

Bamako 1-1 Yanga


Post a Comment

0 Comments