Ticker

6/recent/ticker-posts

Jean Baleke aandaliwa dozi maalum Simba SC

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Othos Baleke ameandaliwa  Program maalum itakayomuongezea kasi ya kufunga mabao akiwa na Kikosi cha Simba SC, kinachojiandaa na mchezo wa Mzunguuko wasita wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.


Simba SC itacheza mchezo huo wa mwisho wa Hatua ya Makundi dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, utakaopigwa April Mosi katika Uwanja wa Mohamed V,  mjini wa Casablanca.


Programu hiyo maalum kwa Baleke ni katika kuhakikisha Mshambuliaji huyo anakuwa tishio katika Ligi ya Mabingwa Afrika, baada kuisaidia Simba SC kuchomoza na ushindi mkubwa wa 7-0 dhidi ya Horoya AC ya Guinea.


Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anaamini ubora na kiwango cha Mshambuliaji huyo, lakini bado anahitaji vitu vichache vya kumuongezea, ili aendelee kuwa tishio katika Michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara.


Robertinho amesema tayari ameanza kumpa Program hizo Baleke tangu timu hiyo, ilipoingia kambini Ijumaa (Machi 24) huko Ndege Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Ameongeza kuwa kingine atakachokifanya ni kutengeneza muunganiko mzuri kati yake ya viungo Clatous Chama, Saidi Ntibanzokiza, Kibu Denis, Sadio Kanoute na Moses Phiri.


“Licha ya Baleke kufunga mabao mawili katika mchezo uliopita dhidi ya Horoya AC, lakini anahitaji kutengenezwa zaidi ili kuhakikisha anazitumia nafasi nyingi ambazo anazozipata.”


“Hivyo ni lazima nimuongezee baadhi ya vitu muhimu vitakavyomfanya aendelee kufunga zaidi, kama unavyofahamu tupo katika mashindano makubwa, ni lazima tuwe bora kila sehemu.”


“Ninataka kumuona Baleke akiendelea kufunga zaidi katika michezo ijayo, hilo linawezekana kwake kwani ana kiwango bora,” amesema Robertinho.


Baleke ni kati ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC, wakati wa Dirisha Dogo msimu huu kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu ya ya ushambuliaji ya klabu hiyo.


Bernard Morrison Kamili Kuwavaa Simba SC Ligi Kuu

Post a Comment

0 Comments