Ticker

6/recent/ticker-posts

Bernard Morrison Kamili Kuwavaa Simba SC Ligi Kuu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

RIPOTI kutoka kambi ya Yanga zinaeleza kwamba Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison huenda akauwahi mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, kufuatia ripoti kueleza ameshapona kwa asilimia 80.


Morrison kwa kipindi kirefu amekuwa nje ya kikosi cha Young Africans kwa sababu za kuwa majeruhi, lakini ameshaanza mazoezi binafsi, huku akitarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake wakati wowote kuanzia sasa.


Ripoti iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Ally Kamwe imeeleza mambo ni mazuri kwa Morrison na wachezaji kama Denis Nkane ambao walikuwa majeruhi na tayari wameshaanza mazoezi.


“Wachezaji ambao wamebaki kwenye timu kwa kutoitwa kwenye timu zao za taifa wanaendelea vizuri na mazoezi na wale waliokuwa majeruhi wapo sawa.”


“Nkane yeye ameshapona na yupo tayari kucheza michezo ya ushindani na kwa Morrison yeye amepona kwa asilimia 80, nafikiri kwenye michezo ijayo ya ligi anaweza kuwa sehemu ya timu,” amesema.


Young Africans kwa sasa inajiandaa na mchezo wake wa mwisho wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa DR Congo. Baada ya hapo itarudi kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Geita Gold FC, kisha maandalizi ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba SC yataanza rasmi na Morrison anaweza akawepo kwenye mchezo huo.

Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo March 27, 2023

Post a Comment

0 Comments