Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yaomba radhi kwa mashabiki kufuatia kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Raja Casablanca

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 


Klabu ya Simba imewaomba radhi wanachama na mashabiki wake kufuatia kichapo cha mabao 3-0 walichokipata siku ya jana katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.


Kupitia kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii, Simba imetoa shukrani kwa mashabiki wake kujitokeza uwanjani na kuwaomba radhi kufuatia matokeo hayo na kusema kuwa wamejifunza na watafanyia kazi mapungufu yote yaliojitokeza katika mchezo huo.


“Shukrani kwa mashabiki na wapenzi wetu. Simba SC inapenda kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi na kujaza uwanja, pia hata wale ambao hawakuja uwanjani”


“Tunawaomba radhi kwa matokeo. Tunaamini tumejifunza na tutaimarika kwa kufanyia kazi mapungufu kwani haya ni mashindano.”


Aidha Simba SC imewaomba wanachama na mashabiki wake kuendelea kuipa ushirikiano timu hiyo


“Tunawaomba muendelee kuipa ushirikiano timu yenu kwani sisi Simba SC tunaamini kwenye nguvu moja”


Mchezo unaofata, Simba watakuwa ugenini nchini Uganda kuvaana na Vipers SC, Februari 25, 2023.Kaze: Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya TP Mazembe


Post a Comment

0 Comments