KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema ari waliyo nayo wachezaji wa timu hiyo ni kiashiria tosha cha kuibuka na ushindi dhidi ya TP Mazembe.
Wakati akihojiwa, kocha huyo amesema maandalizi ya mchezo huo upande wa kiufundi yamekamilika, wanasubiria muda wa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
“Tunawaheshimu Mazembe kwa ukubwa wao, lakini hatupo tayari kupoteza pointi tatu mbele ya mashabiki wetu, naamini utakuwa mchezo mzuri na tutaibuka washindi,” amesema Kaze.
Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo February 19, 2023
0 Comments