Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Sc Wakanusha Kumtimuwa Robertinho

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Simba SC umekanusha taarifa za kutimuliwa kwa Kocha Mkuu wa Kikosi cha Klabu hiyo Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

Taarifa za kutimuliwa kwa Kocha huyo zilichukua nafasi kubwa sana katika Mitandao ya Kijamii, saa chache baada ya mchezo wa Mzunguuko wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uliochezwa Jana dhidi ya Azam FC na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Simba SC imekanusha taarifa hizo kupitia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, huku ikisisitiza Kocha huyo kutoka nchini Brazil bado ni Mwajiriwa halali klabuni hapo, na anaendelea na kazi za kukiandaa kikosi kuelekea mchezo wa Mzunguuko watatu Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC.

“Taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu mkataba wa Kocha Robertinho sio SAHIHI. Anaendelea na majukumu yake ya kuandaa kikosi kuelekea mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika”, imesema taarifa ya Simba SC

Kikosi cha Simba SC kitacheza dhidi ya Vipers SC Jumamosi (Februari 25) mjini Entebe-Uganda katika Uwanja wa St Merry’s, huku kikipoteza michezo miwili ya awali dhidi ya Horoya AC (Guinea) na Raja Casablanca (Morocco).


Mastaa Yanga wapewa Sh130 milioni baada ya kuifunga TP Mazembe

Post a Comment

0 Comments