Ticker

6/recent/ticker-posts

Mgunda: Ntibazonkiza atatusaidia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

KOCHA msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema uwepo wa Saido Ntibazonkiza unampa uhakika wa kuvuna pointi tatu katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Jumamosi hii.


Kocha huyo ameeleza kuwa hiyo ni kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao mchezaji huyo katika mashindano hayo makubwa.


“Nimchezo mgumu kutokana na rekodi ya wapinzani wetu kwenye mashindano haya lakini tunaini letu kubwa lipo kwa Saido sababu kwenye kikosi chetu yeye ndio mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kuwazidi wengine hata mchezo uliopita dhidi ya Horoya AC kama angekuwepo tunaamini angefanya jambo,” amesema Mgunda.


Simba inayoshika nafasi ya tatu kwenye Kundi C, Jumamosi hii itakuwa nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Raja Casablanca ambao tayari wametua nchini leoHabari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 17, 2023

Post a Comment

0 Comments