Ticker

6/recent/ticker-posts

Ahmed Ally - Simba imepungua ubora

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa



Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally, amesema kuna baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wamefanya kazi kubwa kwa miaka mitano mfululizo kwenye michuano ya kimataifa, Ligi Kuu na michuano mingine, hivyo kama binadamu hawawezi kuwa na uwezo, kiwango au ubora ule ule waliokuwa nao awali.


Wakati akihojiwa amesema “Simba imepungua ubora kidogo, lazima tuwe wakweli. Kwanza kuna nyota wetu ambao ubora wao umepungua kidogo kwa sababu ya kuchoka, wamefanya kazi kubwa kwa miaka 5, wamecheza sana kwa miaka yote hiyo michuano ya kimataifa, Ligi kuu na michuano mingine”, - ahmed ally_ Meneja Mawasiliano 


Akatoa mfano mchezaji kama   Mohamed Hussein 'Tshabalala', ambaye anacheza hatua ya awali ya michuano ya kimataifa, hatua ya kwanza, mechi sita za makundi na robo fainali kwa miaka mitatu, haiwezekani baada ya hapo atakuwa kwenye kiwango kile kile, ni lazima kitapungua kidogo.


Mbali na hilo alisema wapo baadhi ya wachezaji ambao walikuwa bora, lakini wameondoka kwenye klabu hiyo kwa kuuzwa.


"Kingine ambacho unaweza kuona ubora huo umepungua kidogo kwenye timu yetu, wapo watu wameondoka kwenye timu yetu, ama wameuzwa, au viwango vyao vilipungua, wakauzwa.


Mohamed Hussein 'Tshabalala', anacheza hatua ya awali ya michuano ya kimataifa, hatua ya kwanza, mechi sita za makundi na robo fainali kwa miaka mitatu, usitegenee baada ya hapo atakuwa kwenye kiwango kile kile, ni lazima kiwango kitapungua kidogo.


Hata hivyo, baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba wamegawanyika kuhusu timu yao ambayo Jumamosi iliyopita ilichapwa mabao 3-0 dhidi ya Raja Casablanca, mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


Baadhi wanamlaumu Kocha Mkuu, Robert Oliveira kuwa upangaji wake usio sahihi na mfumo wake mgumu ndiyo uliosababisha kipigo hicho, wengine wakidai kuwa aina ya wachezaji wengi waliopo kwenye kikosi umri wao ni mkubwa, hivyo kutoweza kuendana na falsafa ya kocha, na wapo walioenda mbali zaidi waliodai karibuni nusu nzima ya wachezaji hawana viwango vya kuichezea timu hiyo, hivyo kikosi kinahitajika kisukwe upya msimu ujao.


Kwa upande mwingine kocha mkuu wa simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wachezaji kwa kupambana kutafuta alama tatu katika mchezo dhidi ya Azam Fc ingawa hatukufanikiwa. Tulitamani kupata pointi zote tatu lakini lazima tukubali tulichojaaliwa na huu ndio mpira.


“Baada ya kuruhusu bao la mapema kipindi cha pili tulibadili mfumo na kutumia washambuliaji watatu ili kuongeza presha na kuwafanya Azam kufanya makosa.


“Tulimuingiza Jean Baleke, Habib Kyombo na Kibu Denis na kuwatoa Pape Sakho, Saido Ntibazonkiza na John Bocco ambao waliongeza kasi na tulibadili hali ya upepo na kupata bao la kusawazisha,” amesema Robertinho.


Robertinho amewapongeza mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ingawa hatujapata matokeo ya kufurahisha.



Mgunda: Ntibazonkiza atatusaidia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

Post a Comment

0 Comments