Ticker

6/recent/ticker-posts

Mamadou Doumbia mashabiki Tulieni Mimi sio mtu wa maneno sana

 

Beki mpya wa Yanga Mamadou Doumbia amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa yeye sio mtu wa maneno sana bali ni mtu wa vitendo zaidi uwanjani.


Doumbia amesajiliwa na Yanga akitokea katika timu ya Stade Malien ya nchini Mali kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.


“Nimefurahi sana kufika hapa, Yanga ni klabu kubwa sana kule Mali, inafatiliwa na watu wengi hivyo kuja hapa ni jambo kubwa sana kwangu kama mchezaji.


“Mimi sio mtu wa maneno sana, kazi yangu ni uwanjani na mashabiki wategemee mazuri kutoka kwangu, nawapenda sana,” alisema Doumbia


Yanga imeendeleza rekodi yake ya kufunga bao kwenye kila mechi ya ligi kwa msimu huu, ikifikisha mabao 39.


Ushindi dhidi ya Ruvu Shooting umewafanya Yanga kufikisha alama 53 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya NBC kwa tofauti ya pointi sita zaidi ya Simba inayofuata ikiwa nazo 47 nafasi ya pili.


Post a Comment

0 Comments