Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal Kuwakabiri Manchester City Leo Katika Kombe La FA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

VIGOGO wa Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal na Manchester City leo usiku watavaana katika mchezo wa raundi ya 32-bora ya Kombe la FA katika Uwanja wa Etihad.


Utakuwa mtihani mkali kwa vijana wa kocha Mikel Arteta ambao wamepoteza michezo mitano mfululizo dhidi ya City katika mashindano yote.


Kwa mara ya mwisho Arsenal walipata ushindi ugenini dhidi ya City kwenye Kombe la FA ni mwaka 1971. 


Walinyamazisha City 2-1 Aprili 2017 na 2-0 Julai 2020 katika michuano miwili iliyopita ya nusu-fainali.


Washikilizi wa mataji mengi ya Kombe la FA, Arsenal (14), huenda wakampa sajili mpya Jakub Kiwior fursa ya kuonja mechi yake ya kwanza dhidi ya City.


Beki huyo alijiunga na Arsenal Jumatatu kutoka Spezia.


Arteta anatarajiwa kufanyia kikosi chake mabadiliko dhidi ya City ikiwemo kuanzisha sajili mwingine mpya Leandro Trossard alitokea Brighton.


“Naona mchezaji (Trossard) ambaye yuko tayari kufanya mambo makubwa na asiye na wasiwasi, hasa katika maeneo ya hatari,” alisema Arteta.


“Ni kitu ambacho tulihitaji katika timu yetu na alidhihirisha uwezo wake alipotusaidia kutamba katika mechi iliyopita,” alisema Arteta.


Emile Smith Rowe anatumai kuanzishwa kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kupona jeraha la kinena.Arteta anajikuna kichwa kuhusu kipa atakayemuanzisha, ingawa mara nyingi Mwamerika Matt Turner amekuwa michumani katika mashindano ya makombe badala Aaron Ramsdale anayetumia zaidi ligini.


City waliosha Chelsea 4-0 nao Arsenal wakapapura Oxford United 3-0 katika michuano ya raundi ya 64-bora.


Macho yatakuwa kwa washambulizi Erling Haaland na Eddie Nketiah kuongoza City na Arsenal katika utafutaji wa mabao mtawalia.


Vikosi vitarajiwa:


Manchester City – Ortega; Walker, Dias, Akanji, Ake; Silva, Rodri, De Bruyne; Mahrez, Haaland, Alvarez.


Arsenal – Turner; Tomiyasu, Holding, Gabriel, Tierney; Vieira, Partey, Xhaka; Trossard, Nketiah, Smith Rowe.


Post a Comment

0 Comments