Ticker

6/recent/ticker-posts

Aucho Wiki Moja Nje

 


Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Khalid Aucho amepata jeraha la mguu wake wa kushoto na atakuwa nje kwa kipindi cha wiki moja.


Kwa mujibu wa vipimo vilivyosimamiwa na daktari wa Yanga, Moses Etutu, Aucho hajavunjika bali ni mshipa wa mguu umevimba baada ya mshituko alioupata akiwa mazoezini.


Mwanzo tulidhani shida ni kubwa kidogo lakini baada ya vipimo tumegundua hajavunjika bali mshipa tu umevimba, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki moja tu,” amesema  Daktari.


Kwa muda huo Aucho anaweza kukosa mechi zisizopungua mbili zaidi za timu yake kuanzia ile ya Jumamosi Januari 21 dhidi ya Ruvu Shooting wakati akiuguza jeraha hilo.


Mashabiki Na Wanachama Wa Simba Wameombwa Kuwa Watulivu


Post a Comment

0 Comments