Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi Za Soka Barani Ulaya January 19,2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Paris St-Germain walikuwa tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, ajiunge na Liverpool msimu uliopita wa joto lakini alikataa mpango huo huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha na Real Madrid . (mirror)


West Ham wametoa ofa kwa mshambuliaji wa Aston Villa Mwingereza Danny Ings, 30, kwa nia ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji huku timu inayokabiliwa na hatari ya kushuka daraja ikihangaika kutafuta mabao. (Telegraph)


Arsenal hawatoshinikizwa  kununua wachezaji  Januari baada ya kumkosa winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 22, aliyehamia  Chelsea na wako tayari kusubiri hadi msimu wa joto kabla ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Uingereza Declan Rice, 24. (Sun).


West Ham ilijaribu kumsajili mlinzi wa Uingereza Harry Maguire, 29, kwa mkopo lakini uhamisho wao ukakataliwa na meneja wa Manchester United Erik ten Hag, ambaye ana nia ya kumbakisha nahodha wa klabu yake Old Trafford kwa muda wote uliosalia.(Mail)


Everton huenda ikashawishiwa kuziba  nafasi ya meneja Frank Lampard, 44, na kocha wa zamani David Moyes, 59, licha ya nafasi ya Mskoti huyo katika klabu ya West Ham kuwa hatarini, huku klabu zote mbili zikiwa kwenye hatari ya  kushushwa daraja la Premier League. (Sun)


Moyes atatimuliwa iwapo West Ham itapoteza mchuano wao wa kushuka daraja katika Ligi ya Premia dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa London Jumamosi. (Telegraph )


Manchester United wamewasilisha ofa ya kandarasi iliyoboreshwa kwa kinda wa Argentina Alejandro Garnacho, 18 huku kukiwa na nia ya kutoka kwa Real Madrid. (Independent)


Fulham inahusishwa na kutaka kumnunua mshambuliaji wa zamani Josh Maja, 24, kwa pauni milioni 4. Mshambulizi huyo wa Nigeria, mzaliwa wa London, ambaye alikuwa kwa mkopo Craven Cottage mwaka 2021, amefunga mabao 11 katika mechi 19 alizoichezea Bordeaux kwenye Ligue 2 ya Ufaransa msimu huu. (Sun)


Atletico Madrid wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 28, kwa ada ya £2.6m. (Fabrizio Romano)


Chelsea na Manchester United wako tayari kuchuana na Tottenham kwa ajili ya kumsajili kipa wa Brentford na Uhispania David Raya, 27, msimu huu wa joto. (Telegraph)


Tottenham wametoa ofa ya pauni milioni 30 pamoja na nyongeza kwa mlinzi wa Sporting Lisbon na Uhispania Pedro Porro, 23, lakini klabu hiyo ya Ureno inataka wafikie kipengele cha kuachiliwa kwa jumla cha £39m.(Record)


FC Copenhagen imethibitisha mazungumzo na Leicester City kuhusu uhamisho wa mlinzi wa kushoto wa Denmark Victor Kristiansen, 20, lakini walisema kwamba makubaliano si ya uhakika. (Leicester Mercury)


Beki wa Barcelona na Uhispania Sergio Busquets, 34, amekataa nafasi ya pauni milioni 17 kwa mwaka ya kujiunga na Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia. (Catalunya Radio)


Mtoto wa Ronaldinho Joao de Assis Moreira anafanya majaribio katika klabu ya zamani ya babake Barcelona . Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 17 hadi sasa ameshindwa kuwafurahisha wakufunzi, lakini rais wa klabu Joan Laporta ameomba apewe muda zaidi. (La Gazzetta dello Sport)


Blackpool wanatazamiwa kumgeukia kocha wa zamani wa Ipswich, Sunderland na Wolves Mick McCarthy kama meneja wao mpya kufuatia kutimuliwa kwa Michael Appleton siku ya Jumatano. (Sun)


Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumapili 15.01.2023Post a Comment

0 Comments