Ticker

6/recent/ticker-posts

Ronaldo atoa tamko kali baada ya kuwekwa benchi dhidi ya Uswizi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameweka wazi msimamo wake kuhusu timu ya taifa ya Ureno, huku kukiwa na taarifa kwamba alikuwa tayari kuondoka kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuwekwa benchi katika mechi ya mwisho ya kufuzu robo fainali dhidi ya Switzerland.

Kauli ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ilikuja saa chache baada ya shirikisho la soka la Ureno pia kutoa taarifa ya kufuta taarifa zozote za uongo.

Siku ya Jumatano, Desemba 7, kulikuwa na ripoti kali kutoka kwa vyombo vya habari vya Ureno zikipendekeza Ronaldo angeweza kuondoka kwenye timu yake katikati ya Kombe la Dunia, kwa sababu hakuridhika na kuwekwa benchi.

Mchezaji huyo alicheza dakika 17 tu  kabla ya mechi kukamilika na video zilizosambazwa zilimuonesha akiwa hana furaha kabisa na kutoka nje ya uwanja mapema kabla ya wachezaji wenza.

Ureno walifuzu robo fainali baada ya kuinyuka Uswizi kibano cha mabao 6 kwa moja, kinda Goncalo Ramos aliyechukua nafasi ya Ronaldo akifunga mabao matatu maarufu Hattrick.

Baada ya taarifa hizo za kuyumbisha kambi ya timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo amekuja wazi na kunyoosha maelezo huku akifutilia mbali uwezekano wowote wake yeye kusikia vibaya sababu ya kuketishwa benchini ili vijana wadogo wacheze.

“Kundi lisilo karibu sana kuweza kuvunjwa na vikosi vya nje. Taifa lililo jasiri sana kujiacha liogopeshwe na adui yeyote. Timu kwa maana halisi ya neno, ambayo itapigania ndoto hadi mwisho! Amini pamoja nasi! Nguvu, Twende Ureno!,” Ronaldo aliandika.

Ikumbukwe wakati wa mahojiano yake ya Piers Morgan siku chache kabla ya kuanza mechi za Kombe la dunia, Ronaldo alisema kuwa ndoto yake kuu itakuwa ni kuona Ureno inafanya vizuri na hata kubeba ubingwa wa dunia – bila kujali ni mchezaji yupi atakayefunga mabao.

Post a Comment

0 Comments