Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA LA FIFA QATAR 2022:Ufaransa yaungana na Uholanzi kutinga robo fainali baada ya kuitandika Poland 3-1

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mabao mawili ya Kylian Mbappe na moja la Olivier Giroud yamewawezesha  mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ufaransa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuitandika Poland 3-1.

Olivier Giroud ameibuka mfungaji bora wa mabao Ufaransa huku mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia wakitandika Poland na kutinga robo fainali. 

Katika mechi hiyo Kylian Mbappe alitoa pasi kwa Giroud ambaye alifunga bao la kihistoria kabla ya Mbappe kufunga mawili na kusaidia Ufaransa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Poland. 

Mshambulizi huyo wa AC Milan alifungia Ufaransa bao lake la 52 na kuvunja rekodi ya raia mwenzake gwiji Thierry Henry. 

Giroud alifunga bao hilo la kihistoria katika dakika ya 44 baada ya kudhibiti pasi ya Mbappe kabla ya kupachika mpira wavuni na kumwacha kwa mataa mlinda lango Wojciech Szczesny. 

Baada ya kuchangia bao la kwanza, Mbappe mwenye kipaji cha kuchana nyavu, alifunga mabao mawili katika kipindi cha pili. 

Mbappe alionja wavu katika dakika ya 74 kuongezea lingine la ushindi katika dakika za lala salama huku akifikisha jumla ya mabao tisa katika mechi 11 pekee za Kombe la Dunia. 

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 23, kwa sasa amefunga mabao 16 katika mechi 14 za awali akiwa na Ufaransa na 33 kwa jumla katika mechi 63. 

Ufaransa sasa itamenyanyana na mshindi atakaye patikana leo kati ya Uingereza na Senegal Jumamosi ijayo. 

Post a Comment

0 Comments