Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA LA FIFA QATAR 2022: Ratiba ya raundi ya mtoano baada ya makundi kukamilika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Michezo ya mwisho ya hatua ya makundi la Kombe la Dunia ilikamilika Siku ya Ijumaa jioni katika jiji la Doha, nchini Qatar.

Jumla ya mechi nne zilichezwa siku ya Ijumaa ambapo timu nne zilifuzu kuingia raundi ya mtoano huku timu zingine nne zikikusanya virago na kulejea nyumbani baada ya kuondoshwa kwenye mashindano.

Ghana na Cameroon za Afrika, Serbia ya Ulaya na Uruguay ya Amerika Kusini ni timu ambazo zimeondoshwa kwenye mashindano ya kombe hilo siku ya Ijumaa huku Ureno,Korea Kusini Uswizi na Brazil zikifuzu kusonga mbele.

Brazil iliweza kumaliza katika kilele cha kundi G licha ya kupoteza 0-1 dhidi ya Cameroon. Switzerland ilichukua nafasi ya pili ya kundi hilo baada ya kuilaza Serbia 3-2.

Hapo awali Ureno ilichukua uongozi wa kundi H licha ya kupigwa 2-1 na Korea Kusini ambayo ilichukua nafasi ya pili.  Licha ya Uruguay kuipiga Ghana 2-0 haikuweza kufuzu kuingia raundi ya muondoano huku ikichukua nafasi ya tatu nayo Ghana ikishika mkia.

Ghana, Cameroon, Serbia na Uruguay ziliungana na timu zingine kumi na mbili katika safari ya kurudi  nyumbani ya mapema. Timu kumi na mbili ambazo zilitimuliwa hapo awali ni pamoja na Qatar, Ujerumani, Ubelgiji, Costa Rica, Saudi Arabia, Mexico, Tunisia, Denmark, Iran, Wales, Ecuador na Canada.


Timu  zilizosalia zitamenyana kati ya Jumamosi ,Desemba 3, na Jumanne Disemba 6 ili kubaini watakaofuzu kuingia robo fainali.

Hii hapa ratiba ya Michuano hiyo: 


Disemba  3:

Uholanzi  vs Marekani - 6PM

Argentina vs Australia- 10PM


Disemba 4:

Ufaransa vs Poland - 6PM

Uingereza vs Senegal - 10PM


Disemba 5:

Japan vs Croatia - 6PM

Brazil vs Korea Kusini - 10 PM


Disemba 6:

Morocco vs Uhispania- 6PM

Ureno vs Uswizi - 10pm

Post a Comment

0 Comments