Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA LA FIFA QATAR 2022: Ghana na Cameroon zatupwa nje ya Michuano hiyo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Timu ya Ghana imeaga michuano ya kombe la dunia baada ya kufungwa na Uruguay bao 2-0, mabao ya Uruguay yalifungwa na De Arrascaeta katika dakika ya 26 na Giorgian katika dakika ya 32.

Washabiki wa  Ghana walikuwa na matumaini makubwa na timu yao kupata ushindi lakini Uruguay ilionyesha ubora mkubwa na kuchukua ushindi katika mchezo huo.

Hadi mwisho wa mchezo Uruguay pia ilijikuta pamoja na ushindi lakini wote pamoja na Ghana wakitolewa nje ya michuano hiyo.

Korea Kusini yaingia raundi ya pili na kuishangaza Ureno

Kombe la dunia la mwaka huu limejaa maajabu ambapo timu ya Korea kusini ilifanya maajabau kwa kuifunga Ureno bao 2-1.

Korea Kusini ilikuwa nyuma kwa bao moja ikasawazisha na kuongeza la ushindi.

Cameroon yaiumbua Brazil lakini yatolewa

Alikuwa ni nahodha Vincent Aboubakar mshambuliaji hatari wa Cameroon aliyepachika bao la kwanza na la ushindi kwa timu yake katika dakika za majeruhi na kuipa ushindi Cameroon.

Bao hilo lilifungwa kwa kichwa na kuharibu sherehe ya Wabrazil waliokuwa wakiimba wakati wote wa mechi hiyo katika Uwanja wa Lusail.

Nahodha huyo wa Cameroon alishangilia kwa kuvua shati lake. Kwa bahati mbaya, Aboubakar alisahau kwamba tayari alipata kadi ya njano na alitolewa nje baada ya kupokea njano ya pili kwa kusheherekea huko.

Lakini kwa bahati mbaya ushindi wao haukuweza kuwapeleka raundi ya pili baada ya timu ya Uswissi kuitandika Serbia kwa bao 3-2.

Kwa maana hiyo kundi hilo ambalo tayari Brazil alikuwa ameshafanikiwa kukata tiketi yake anaungana na Switzerland kuelekea rundi ya 16.

Mchezaji wa Brazil na Arsenal Gabriel Martinelli alipata nafasi nzuri zaidi kipindi cha kwanza kwa mpira wa kichwa uliogonga vizuri dakika ya 14 lakini golikipa Devis Epassy aliokoa kwa ustadi wa hali ya juu , Martinelli hata hivyo aliisumbua sana ngome ya Cameroon.


Brazil sasa itakwaana na Korea Kusini

Golikipa wa akiba wa pili wa Cameroon Devis Epassy aliyechaguliwa kuendelea baada ya kipa nambaro mpja Andre Onana kuondolewa kwenye timu hiyo alithibitisha kuwa ni bora kwani alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya hatari ya Brazil iliyoelekezwa golini kwake na washambuliaji wa Brazil wakiongozwa na Gabrielle Martinelli.

Hadi mwisho wa mchezo Cameroon moja Brazil bila. Kutokana na hayo sasa Brazil inaelekea katika raundi ya 16 ambapo itakumbana na vijana machachari wa Korea Kusini ambapo wachambuzi wanasema itakuwa mechi ya kuvutia.

Siku ya Jumamosi Marekani watafungua na Uholanzi katika raundi ya 16 na Argentina anapambana na Australia -Socceroos moja ya timu zilizoshangaza katika kombe hili la dunia ikiwa haina majina makubwa lakini imeweza kufanya vyema.

Na siku ya Jumapili Ufaransa inapambana na Poland wakati wawakilishi wa Afrika Senegal wanapambana na Uingereza.


Serbia yatolewa na Uswissi

Nayo timu ya Serbia ilipambana vikali na Uswisi ikiwa inawania kuingia raundi ya 16 na ilifanikiwa baada ya ushindi wa bao 3-2 .

Mabao ya Uswisi yalifungwa na Xhedan Shakiri katika dakika ya 20 Breel Emboro dakika ya 44 na Remo Freuler dakika ya 48.

Serbia imekua ikizalisha wachezaji mahiri zaidi barani Ulaya, wengi wao wakicheza katika ligi kuu za bara hilo, lakini kwa mara nyingine, wamefanya vibaya kwenye Kombe la Dunia na kutolewa katika hatua ya makundi.

Mbali na fowadi wa Fulham, Aleksandar Mitrovic, ambaye alifunga mabao matatu nchini Qatar, kikosi cha Serbia cha Dragan Stojkovic kimeshindwa kufanya lolote la kutisha.

Post a Comment

0 Comments