Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Bruno Fernandes Abeba Ureno Dhidi Ya Uruguay Katika Kundi G

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

URENO wametinga hatua ya 16-bora kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kuifunga Uruguay 2-0 katika pambano la Kundi H katika dimba la Lusail Iconic, Qatar.

Kiungo mzoefu wa Manchester United, Bruno Fernandes, alifungulia Ureno ukurasa wa mabao katika dakika ya 54 baada ya kumzidi maarifa kipa Sergio Rochet ambaye pia aliwajibishwa vilivyo na fowadi Cristiano Ronaldo.

Ushindi wa Ureno unaacha Uruguay katika wakati mgumu sana sasa inabidi waifunge Ghana katika mchuano wao wa mwisho wa Kundi H ili kufuzu kwa raundi ya mtoano.

Nusura Rodrigo Bentancur asawazishie Uruguay katika dakika ya 70 ila kombora lake likadhibitiwa vilivyo na kipa Diogo Costa wa Ureno. Maxi Gomez naye alishuhudia fataki yake ikibusu mhimili wa goli la Ureno ambao sasa wanajivunia alama sita, tatu kuliko Ghana wanaokamata nafasi ya pili. Uruguay na Korea Kusini wana alama moja kila mmoja.

Fernandes alifungia Ureno bao la pili mwishoni mwa kipindi cha pili kupitia penalti iliyochangiwa na Jose Gimenez aliyemwangusha kiungo huyo wa zamani wa Sporting ndani ya kijisanduku.

Ushindi kwa Ureno dhidi ya Uruguay unatarajiwa sasa kuwaweka pazuri kutandika Korea Kusini katika pambano lao la mwisho la Kundi H mnamo Disemba 2, 2022 na kudhibiti kilele. Ufanisi huo utawadumisha kileleni mwa Kundi H na hivyo kukutana na kikosi kitakachoambulia nafasi ya pili katika Kundi G linalojumuisha Brazil, Uswisi, Cameroon na Serbia.

Uruguay waliotoshana nguvu na Korea Kusini kwa sare tasa mnamo Novemba 24, 2022, waliwahi kukutana na Ureno katika hatua ya 16-bora kwenye Kombe la Dunia mnamo 2018 nchini Urusi na wakajizolea ushindi wa 2-1.

Uruguay walitwaa Kombe la Dunia mnamo 1930 na 1950. Waliibuka wa nne kwenye kipute hicho mnamo 2010 nchini Afrika Kusini kabla ya kuaga fainali za 2014 katika raundi ya 16-bora nchini Brazil na kutinga robo-fainali miaka minne iliyopita nchini Urusi.

Post a Comment

0 Comments