Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia la FIFA 2022: Ghana Yakaza Hadi Mwisho na Kuifunga Korea Kusini 3-2

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Timu ya taifa ya Ghana imepambana hadi mwisho na kufanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia yanayoendekea nchini Qatar. 

Baada ya kupoteza mechi yao ya kwanza kundi H 3-2 dhidi ya Ureno, Ghana wamejikaza kisabuni na kusajili ushindi sawia (3-2) dhidi ya Korea Kusini. 

Black Stars walielekea katika mapumziko wakiwa uongozini 2-0 lakini wakarejea na kulegeza kmba, Korea wakifunga mabao mawili katika dakika tatu na kusawazisha. 

Baada ya pande zote kushambulia huku Korea Kusini ikionekana kuwa na madude hatari zaidi, ni Ghana waliotangulia kuona lango la mwengine.

Mohammed Salisu alitikisa wavu katika dakika ya 24 kabla ya Mohammed Kudus kufanya mambo kuwa 2-0 dakika kumio baadaye. 

Baada ya mapumziko, straika wa Korea Kusini Joe Gue-sung alifunga mabao mawili ya kichwa katika dakika ya 58 na 61 na kufanya mambo kuwa sare. 

Kudus hata hivyo alirejea dakika za 68 na kupiga bao lake la pili na la tatu kwa Ghana - Black Stars wakisajili ushindi wao wa kwanza katika Kombe la Dunia nchini Qatar. 

Kocha wa Korea Kusini Paulo Bento amelimwa kadi nyekundi na refa wa Uingereza Anthony Taylor mwishoni mwa mchezo. 

Bento ambaye ni raia wa Ureno alimwandama Tylor kwa kumaliza mechi wakati walikuwa wamepata kona ambaye ilikuwa fursa nzuri ya kusawazisha. 

Post a Comment

0 Comments