Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia fifa 2022: Cameroon Wagawana Alama na Serbia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Miamba wa soka barani Afrika Cameroon wametoka mabao mawili nyuma na kunusuru alama muhimu katika mechi yao dhidi ya Serbia katika mechi ya Kombe la Dunia nchini Qatar. 

Licha ya kuchukua uongozi mapema, the Indomitable Lions wamehitajika kutoka nyuma kwa mabao mawili ili kulazimisha sare ya 3-3 dhidi ya Serbia katika uwanja wa Al Janoub. 

Cameroon walichukua uongozi katika dakika ya 29 baada ya beki Jean-Charles Castelletto kucheka na wavu mbele ya mashabiki 39,789. 

Serbia hata hivyo walipiga mabao mawili katika muda wa nyongeza katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Strahinja Pavlovic na Sergej Milinkovic-Savic. 

Kipindi cha pili Serbia walirejea katika kipindi cha pili na kupiga bao safi kupitia kwa Aleksandar Mitrovic katika dakika ya 53 na kuaminika kuwa jahazi lao zimezama. 

Kocha wa Cameroon Rigobert Songa alifanya mageuzi katika dakika ya 55 - akimtoa Martin Hongla na nafasi yake kuchukuliwa na Vincent Aboubakar. 

Aboubakar alicheka na wavu katika dakika ya 63 kabla ya kumwandalia pasi Eric Maxim Choupo-Moting na kufanya mambo kuwa 3-3. 

Wababe hao sasa wanahitajika kuwatandika Brazili ili angalau kuwa na nafasi ya kufuzu kwa raundi ya 16 bora. 


Post a Comment

0 Comments