Ticker

6/recent/ticker-posts

''Simba inaogopwa Afrika''-Barbara Gonzalez

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amesema kikosi cha klabu hiyo kimekuwa kikiogopwa na timu zinazopangiwa kucheza nazo kwenye michuano ya kimataifa huku akijinasibu kama klabu wapo tayari kutimiza malengo ya klabu kwa msimu huu

 “Kikosi chetu ni kizuri na tukipewa malengo makubwa  tutayafikia na kule Angola kila wakisikia jina la Simba, Simba walikuwa na hofu na kila nchi Watu wanahofu na Simba, hata Viongozi tuliokuwa nao kule jukwaani wa De Agosto walikuwa na hofu na najua  watakuja hapa wakiwa na hofu dhidi ya Simba”amesema Barbara Gonzalez

Simba imerejea leo kutokea Luanda nchini Angola baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Premiero De Agosto kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku wakitaraji kurejeana Jumapili ya Oktoba 16, 2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments