Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal Yaitandika Liverpool Na Kurejea Kileleni

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KOCHA Mikel Arteta amesema ushindi wa 3-2 walioupata Arsenal dhidi ya Liverpool katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumapili katika uwanja wa Emirates unastahili kuwaaminisha zaidi katika michuano ijayo.

Matokeo hayo yalirejesha Arsenal kileleni mwa jedwali la EPL kwa alama 24, moja mbele ya mabingwa watetezi Manchester City wanaokamata nafasi ya pili.

“Kikosi kinazidi kuimarika na matokeo yanaridhisha. Vijana wanacheza kwa kujituma bila presha yoyote na kila mmoja anatawaliwa na kiu ya kushinda kila mechi,” amesema Arteta.

Ushindi huo – mnono zaidi kwa Arsenal kujivunia muhula huu – ulikuwa wao wa nane kutokana na michuano tisa ya EPL. Liverpool walioambulia sare mbili dhidi ya Brighton (3-3) na Everton (0-0) awali, sasa ni wa 10 jedwalini kwa pointi 10 sawa na Brentford, West Ham United na Everton waliopokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Manchester United.

Arsenal walipata mabao yao kupitia kwa fowadi Gabriel Martinelli na mvamizi Bukayo Saka aliyefunga mawili. Liverpool kwa upande wao walifungiwa na Darwin Nunez na Roberto Firmino.

Post a Comment

0 Comments