Ticker

6/recent/ticker-posts

Nyota wa Juventus Paul Pogba Akiri Kutumia Uchawi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Mchezaji nyota wa Juventus Paul Pogba amekiri kwamba amekuwa akitumia uchawi lakini sio kwa kumroga mchezaji mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappé 
  • Mvamizi huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, aliwaambia maafisa wapelelezi kwamba aliamua kutafuta huduma ya mganga kwa sababu za kibinadamu tu 
  • Kwa mujibu wa ripoti, Paul Pogba amebadilisha nambari yake ya simu mara mbili tangu kuanza kwa kesi hiyo, ili kuepuka jaribio la ulaghai ambao alikuwa mwathiriwa

Paul Pogba amekiri kutumia uchawi katika mahojiano yake ya pili na maafisa wapelelezi wa Ufaransa. 

Mathias Pogba, kaka mkubwa wa Paul alikuwa amefunguka mazito kumhusu mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka wa 2018, akisema amekuwa akijihusisha na ushirikina na pia kumroga mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappé. 

Lakini Paul Pogba amekiri kwamba amekuwa akitumia uchawi kwa sababu za kibinadamu wala sio kwa kumroga Mbappé.

Kwa mujibu wa France Info, Paul aliwafichulia wapelelezi hayo wakati wa alipokuwa akihojiwa tena kwa mara ya pili, akidai kuwa ana ushahidi wa kuthibitisha.

Kiungo huyo wa zamani wa Man United, alidai kwamba alikuwa mwathiriwa wa jaribio la ulaghai ambalo kulingana naye lilipangwa na baadhi ya jamaa zake akiwemo kaka yake mkubwa Mathias Pogba. 

Paul anaendelea kudai kuwa ni mwathiriwa wa jaribio la ulaghai wa pauni 13 milioni na kaka yake Mathias, na marafiki zake wa utotoni ndiyo waliopanga genge hilo. 

Mathias aliwasha moto mtandao wa kijamii na video yake ya dakika tatu siku ya Jumapili, Agosti 28, akiahidi kuchapisha "ufichuzi mkubwa" kuhusu nyota huyo wa zamani wa Manchester United. 

Paul hata hivyo, kwa majibu yake ya haraka kupitia kwa mawakili wake alidai kuwa kaka yake ni mmoja wa genge la uhalifu lililopangwa kumlaghai kitita cha Pauni milioni 13. 

Lakini katika kuongezea chumvi kwenye jeraha, kaka mkubwa wa Pogba alifichua kuwa mdogo wake amekuwa akitumia mamilioni ya pesa katika uchawi ili kujilinda dhidi ya kupata jeraha.


Post a Comment

0 Comments