Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi awataka wachezaji wake kuwa makini wanapo fika langoni, asema wanakosa nafasi nyingi za kufunga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amewataka wachezaji wake kuwa makini wanapofika langoni mwa timu pinzani kwa sababu wanakosa nafasi nyingi nzuri za kufunga wanapokuwa na mpira.

Nabi ameyasema hayo baada ya kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 9-0 dhidi ya Zalan FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma na kutinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo wa kwanza yanga, walipata ushindi wa 4-0 kabla ya kuibuka na ushindi wa 5-0 katika mchezo wa marudiano mkondo wa pili.

Mshambulizi bora wa timu hiyo, Fiston Mayele alifunga hat-trick katika mechi zote mbili.

Baada ya sare tasa katika kipindi cha kwanza, Farid Mussa alifunga bao la kwanza dakika ya 47 kabla ya Stephanie Aziz Ki kuongeza la pili na kutengeneza hat-trick ya Mayele.

“Sijaridhishwa kabisa na namna tulivyocheza hasa kipindi cha kwanza kwa sababu tulikosa nafasi nyingi za kufunga na hivyo kumaanisha bado tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye uwanja wa mazoezi.

"Iwapo utakutana na timu kubwa na ukashindwa kubadili matokeo kutokana na nafasi chache unazotengeneza, basi mchezo unaweza kuwa mgumu kwa upande wako...ndiyo maana nasisitiza kwamba tunapaswa kuboresha uwezo wetu wa kufunga," Nabi alisema.

Aliongeza kuwa mchezaji wake Stephanie Aziz Ki bado hajapata mfumo wake wa kawaida wa uchezaji akisema wachezaji wenzake bado hawajaelewa mfumo wake wa uchezaji hivyo mara tu watakapojuana zaidi, kiwango chake kitaongezeka maradufu.

Pia alimshukuru mgeni rasmi siku hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kwa kuwapa moyo kabla ya mechi akisisitiza kuwa kitendo hicho kizuri kitawafanya wawe na nguvu zaidi.

Nabi aliwataka wale wanaohusika na upangaji wa mechi kuzingatia maisha ya wachezaji kwani hivi karibuni wamekuwa wakijihusisha na michezo ya ushindani kila baada ya siku tatu jambo ambalo alisema si zuri kiafya kwa wachezaji.

“Mfano baadhi ya wachezaji wetu wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikimaanisha kwamba watacheza mechi mbili za kirafiki na baada ya hapo watarejea na kwenda moja kwa moja kutimiza majukumu ya ligi.

"Wachezaji ni binadamu na pia wanahitaji muda wa kupumzika, kwa ajili ya kukuza soka la nchi, wale wanaohusika katika kutengeneza ratiba za mechi wanapaswa kuzingatia na kulinda afya za wachezaji hawa," alisema.

Post a Comment

0 Comments