Ticker

6/recent/ticker-posts

'Dejan Georgijevic' Amuibua Azim Dewji

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mfadhili wa zamani wa Klabu ya Simba, Azim Dewji amesema kuwa nyota wa kimataifa wa Serbia Dejan Georgijevic atawasumbua sana kwenye mashindano ya kimataifa kuliko ligi za ndani.

Dewji alisema Dejan ambaye kwa sasa amekuwa maarufu sana hapa Tanzania anahisi hatofanya vizuri kwenye ligi na mashindano ya ndani kwa sababu wachezaji wa hapa wanakamiana sana lakini kule kimataifa atakutana na wachezaji wanaocheza kwa nafasi na hapo ndipo atawatesa sana.

Akizungumzia uwezo wa Dejan Dewji alisema: “Yule ni mchezaji mzuri ambaye atatusaidia sisi zaidi katika mashindano ya Kimatifa kwa sababu kule atakutana na wachezaji wengine ‘mapro’ ambao wanacheza kwa nafasi nayeye hapo lazima atang’aa.

“Lakini kwa ligi ya hapa nyumbani na mashindano ya ndani hatofanya vizuri kwa sababu wachezaji wetu wanakamiana sana na yeye atachukua muda sana kuweza kuzoea mazingira hayo. Tofauti na hawa wachezaji wengine ambao wamesajiliwa kutoka nchi za Afrika.”

Post a Comment

0 Comments