Ticker

6/recent/ticker-posts

Chipukizi wa Arsenal Ethan Nwaneri Aingia katika Vitabu vya Guinness Records

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


MNAMO Jumapili iliyopita Ethan Nwaneri aliingia kwenye kumbukumbu za historia za Guinness World Records baada ya kuwa mchezaji mdogo zaidi duniani kuwahi kuchezeshwa katika ligi yoyote kuu.

Nwaneri aliweka historia hiyo alipoingia ugani dakika ya 80 katika mechi dhidi ya Brentford, akiwa na umri wa miaka 15 na siku 181.

Kinda huyo amekuwa akinawiri katika akademia ya Arsenal kama kiungo mshambuliaji, nyota yake iking’aa zaidi alipopandishwa hadi kikosi cha wachezaji wasiozidi miaka 18 miezi michache iliyopita, licha ya kuwa na umri mdogo.

Ni ishara ya ustadi wake kwamba kocha Mikel Arteta alimwita kujiunga na timu ya watu wazima mkesha tu wa mechi ya wikendi iliyopita.

Aliingia ugani Brentford Community dakika ya 80 akiwa amevalia jezi nambari 83 na kuchukua nafasi ya Fabio Viera, wakati wa pambano hilo ambalo Arsenal ilipepeta Brentford magoli 3-0.

Kinda huyo alivunja rekodi ya Cesc Fabregas, ambaye alichezea Arsenal kwa mara ya kwanza dhidi ya Rotherham United mnamo Oktoba 2003.

Wakati huo, Arsenal bado walikuwa wakiandaa mechi zao za nyumbani katika uga wa Highbury.

Aidha, Cesc alikuwa miaka 16 na siku 177 wakati huo; alisakatia Arsenal, maarufu The Gunners, mechi 303 na kufunga jumla ya mabao 57.

Ethan hakuwa amezaliwa Cesc akiweka rekodi hiyo kwani alitua duniani Machi 21, 2007, baada ya Gunners kuhamia Emirates mnamo 2006.

Nwaneri sasa pia ndiye mchezaji mdogo kuwahi kusakata boli katika EPL.

Alivunja rekodi ya Harvey Elliot alipowajibishwa na Fulham mnamo Mei 2019 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 30.

Kabla ya Elliot, Jack Wilshere – ambaye kwa sasa ni kocha wa Ethan katika Under-18 ya Arsenal – alishikilia rekodi hiyo.

Wilshere alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 256 alipopewa nafasi katika mechi dhidi ya Black Burn mnamo Septemba 2008.

Nwaneri pia amechezea vikosi vya Under 18 na Under 21 kwa The Gunners.

Arsenal ndicho kikosi kichanga zaidi EPL- umri wa wastani wa 23.8. Inakisiwa Gunners inamlipa Nwaneri pato la Sh18 milioni kila mwezi.

Post a Comment

0 Comments