Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA BINGWA NGAO YA JAMII 2022-2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 


𝗙𝗨𝗟𝗟 𝗧𝗜𝗠𝗘

Young Africans SC 2-1 Simba SC

MABINGWA wa Kihistoria katika Soka la Tanzania, Klabu ya Yanga SC wamefanikiwa kutetea tena taji la Ngao ya Jamii msimu wa 2022/2023 baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya watani zao Simba SC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mabao yote ya Yanga SC yamefungwa na Mshambuliaji, Fiston Mayele dakika 49 na 80, baada ya kupokea asisti safi kutoka kwa Aziz Ki na kufanikiwa kuisawazishia yanga bao la kwanza kabla ya mlinzi Dickson Job kutoa  asisti ya bao la pili baada ya kuichambua ngome ya Simba SC na kufanya mchezo huo kuisha ndani ya dakika 90 pekee.

Katika kipute hicho Yanga SC walionekana bora zaidi katika eneo la Kiungo cha ukabaji kilichokuwa chini ya Yannick Bangala na Khalid Aucho wakiwalinda Mabeki, Kibwana shomari na Dickson Job.


Yanga SC imeanza msimu vyema msimu huu wa mashindano wa 2022-2023 baada ya ushindi huo ambapo August 16,2022 watafungua Pazia la Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati Simba SC wakifungua Ligi hiyo dhidi ya Geita Gold FC katika dimba la Mkapa Stadium, Dar es Salaam August 17,2022.

Post a Comment

0 Comments