Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yairarua Simba, Azizi Ki ageuka Shujaa kwa Mkapa

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KLABU ya Yanga imeanza vema msimu mpya kwa kutetea taji lake la Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mtani wake Simba.

Mabao mawili ya mshambuliaji Fiston Mayele yameiwezesha Yanga kutoka nyuma baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa Simba kwenda mapumziko ikiongoza bao 1-0.

Tangu kipindi cha pili kianze Yanga imeonekana kutumia vizuri maeneo yake ya pembeni ambako kuna wachezaji walioingia kipindi cha pili, Jesus Moloko na Bernard Morrison.

Injini inayoonekana kuwaka Azizi Ki inaonekana kutawala eneo la juu ya kiungo cha Yanga kuwabidi kucheza soka la kwenda mbele zaidi.

Simba inacheza pasi chache kwenda mbele, licha ya mabadiliko kadhaa kufanywa na Zoran ikiwemo kuingia Mzamiru Yassin, John Bocco na Nelson Okwa  yanonekana kushindwa kufua dafu.

Mabao mawili yaliyofungwa na Mayele yametosha kuamsha vaibu kwa mshabiki wa Yanga huku Simba wakinyong'onyea.


Azizi Ki ageuka Shujaa kwa Mkapa

MAVITU anayofanya Aziz Ki yanaonekana kuwakosha mashabiki wa Yanga na kuamua kuanza kuimba jina la raia huyo wa Burkina Faso.

Azizi Ki ndiye mpishi aliyepika bao la kusawazisha kwa Yanga lililofungwa na Fiston Mayele dakia ya 68 ya mchezo.

"Azizi, Azizi," waliskika mashabiki hao wa Yanga mara kwa mara wakiimba jina la staa huyo aliyesajili kutoka ASEC Mimomas ya Ivory Coast, ambapo alimaliza ligi kuu nchini humo akitwaa tuzo ya mchezaji bora.

Tangu aanze kutumika kama namba 10 katika kipindi cha pili anaonekana kuwa na madhra zaidi kwa Simba tofauti na awali ambapo alikuwa akitokea pembeni.

Katika mchezo huo wa fainali ya Ngao ya Jamii kati ya vigogo hao wa Kariakoo imetamatika kwa Yanga kuibuka kidedea kwa mara ya mpili mfululizo huku muuaji akiwa yuleyule Fiston Mayele.

Post a Comment

0 Comments