Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za usajili: Aubameyang Awawekea Ngumu Chelsea; PSG wamuhitaji Rashford

Mshambuliajii wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang amesema anapendelea kuendelea kusalia Camp Nou kuliko kurejea Ligi Kuu ya Uingereza kujiunga na Chelsea.

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel ameweka shinikizo kwa mmiliki mwenza wa klabu hiyo Todd Boehly  kumnunua Aubameyang, baada ya kufanya nae kazi mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal wakati alipokuwa Borussia Dortmund.

Paris Saint-Germain wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford kuhusu uwezekano wa kumsajili katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Manchester United watafanya mazungumzo zaidi na mama na wakala wa Adrien Rabiot baada ya kuafikiana na Juventus uhamisho wa euro milioni 17.

Mahitaji ya Rabiot huenda yakazidi pauni milioni 6 kwa mwaka anazopata Juventus - mshahara unaomfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi Serie A.

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anasema klabu hiyo imekataa ofa mbili kutoka Chelsea kwa ajili ya mchezaji Wesley Fofana.

The Foxes pia wamefanya mazungumzo na Jamie Vardy kuhusu mkataba mpya lakini wameshindwa kumshawishi Youri Tielemans kusalia. Arsenal wanahusishwa na kutaka kumnunua Mbelgiji huyo kwa pauni milioni 25.

Manchester City wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Atletico Madrid, Renan Lodi, huku pia wakifikiria kumnunua Kieran Tierney wa Arsenal.

Juventus wanakaribia kuinasa saini ya fowadi wa Barcelona Memphis Depay, ingawa Tottenham bado hawajatoka katika mbio za kumsajili Mholanzi huyo.

Chelsea huenda ikaingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Nicolo Zaniolo anae windwa na Tottenham kwa kuwapa Roma winga Mmarekani Christian Pulisic kama makubaliano ya kubadilishana wachezaji .

Real Madrid wamefikia makubaliano kabla ya wapinzani wao Atletico kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Iker Bravo.

Nottingham Forest imewasilisha ombi la kwanza kwa mshambuliaji wa Watford Emmanuel Dennis lenye thamani ya zaidi ya £20m.

West Ham wametoa ofa ya awali ya €30m pamoja na nyongeza ya €5m kwa kiungo wa Sporting CP Matheus Nunes - mchezaji ambaye amekuwa akihusishwa mara kwa mara na Liverpool.

Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl amethibitisha kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Che Adams.

Watford, Burnley, Blackburn na Sheffield United ni miongoni mwa vilabu vinavyowania kumsajili Sepp ven den Berg wa Liverpool kwa mkopo.

Marseille wamewasiliana na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo beki wao wa kati Eric Bailly.

Post a Comment

0 Comments