Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba, Yanga kuanzia ugenini CAF

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Hatimaye mbivu na mbichi za wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya CAF imefahamika baada ya droo kufanyika huku timu hizo zikianzia ugenini katika hatua ya awali ambapo ni Azam pekee ndiye ataanzia katika hatua ya Kwanza.

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga watacheza mchezo wao wa awali kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini ambapo Mshindi wa mchezo huo atacheza na mshindi kati ya St. George dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Simba imedondokea mikononi mwa Big Bullet ya Malawi katika mchezo wa awali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo itaanzia ugenini huku mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Red Arrows dhidi ya Premiro Agosto.

Nao Geita Gold wawakilishi wapya wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho ataanzia ugenini dhidi ya Bilal Al Sahil ya Sudan kwenye hatua ya awali huku Azam FC wao wakianzia hatua ya kwanza ambapo wa watacheza na mshindi kati Al Akhder v Al Ahli Khartoum.


Post a Comment

0 Comments