Ticker

6/recent/ticker-posts

Leonel Messi mbioni kuvunja rekodi ya Dani Alves

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

•Maxwell na Andres Iniesta wanashika nafasi ya nne kwa kupata mataji mengi.

•Tangu ajiunge na Paris Saint Germain 2021, Lionel Messi ameongeza mataji mawili kwenye  - Ligue 1 (2021-22) na Trophee des Champions (2022).


Leonel Messi  yuko mbioni kuvunja rekodi ya kuwa na mataji mengi, kwa sasa rekodi hiyo inashikiliwa na Dani Alves ambaye ni mchezaji mwenye mataji mengi zaidi duniani.

Messi kwa sasa amepata mataji 41 katika maisha yake ya soka, ikibakiza taji moja tu kumfikia Dani Alves.

Messi alishinda mataji 35 akiwa Barcelona (2004-2021) huku akishinda mataji manne ya kimataifa, likiwemo la Copa America 2021. Muargentina huyo pia alishinda medali ya dhahabu ya Olimpiki huko Beijing 2008.

Tangu ajiunge na Paris Saint Germain 2021, Lionel Messi ameongeza mataji mawili kwenye  - Ligue 1 (2021-22) na Trophee des Champions (2022).

Dani Alves beki huyo wa Brazil alishinda tuzo yake ya kwanza ya kitaalamu akiwa na klabu ya nyumbani ya Bahia.

Baada ya kushinda mataji matano ndani ya miaka sita akiwa na Sevilla,Beki huyo  alihamia Barcelona kwa pauni milioni 23 na akaendelea kushinda mataji 23 - ikiwa ni pamoja na mataji sita ya La Liga na matatu ya UEFA Champions League.

Baada ya muda mrefu wa kubeba taji akiwa Juventus (2016-17 - mataji mawili), Paris Saint-Germain (2017-19 - mataji sita) na Sao Paulo (2019-21 - kombe moja), Alves amejiunga na timu ya Mexico ya UNAM mwaka huu baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha pili akiwa Barcelona.

Maxwell na Andres Iniesta wanashika nafasi ya nne kwa kupata mataji mengi.

Wawili hao, ambao waliwahi kuwa wachezaji wenza katika klabu ya Barcelona, ​​wana mataji 37 kila mmoja.

Post a Comment

0 Comments