Ticker

6/recent/ticker-posts

Martin Odegaard: Nyota wa Arsenal anakuwa nahodha wa pili mdogo zaidi kwenye Ligi Kuu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Kiungo wa kati wa Arsenal Martin Odegaard amekuwa nahodha wa pili mwenye umri mdogo katika Ligi kuu ya Uingereza.

Odegaard atachukua nafasi ya Alexander Lacazette, ambaye aliondoka Emirates Stadium msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Wanagunners  walicheza na Sevilla katika mechi yao ya mwisho ya kujiandaa kwa msimu Jumamosi, Julai 30.

Walitumia fursa hiyo kumtambulisha Odegaard kama nahodha mpya wa klabu hiyo.

"Tunafuraha kutangaza kwamba Martin Odegaard ameteuliwa kuwa nahodha wetu mpya wa kikosi cha kwanza cha wanaume," taarifa kutoka Arsenal ilisema.

"Odegaard ana uzoefu wa kuvaa kitambaa cha unahodha, akiwa nahodha wa Norway tangu Machi 2021, ambaye ameshinda mechi 43," taarifa hiyo iliongeza.

Kulingana na 'Talk SPORT', Odegaard aliwashinda baadhi ya wagombea na kutwaa nafasi ya unahodha wa Arsenal.

Chapisho hilo linadai kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway amependelewa zaidi ya wagombeaji wengine waliotarajia ushindi huo.

Kieran Tierney, Aaron Ramsdale, na nahodha wa zamani Granit Xhaka wote walikuwa wameungwa mkono kupata kitambaa hicho.

Akiwa na umri wa miaka 23, Odegaard sasa anakuwa nahodha wa pili mwenye umri mdogo zaidi katika  Ligi kuu ya Uingereza pamoja na Lloyd Kelly wa Bournemouth, ambaye pia ana umri wa miaka 23.

Mnamo tarehe 20 Agosti 2021, Arsenal ilitangaza usajili wa kudumu wa Odegaard kutoka Real Madrid kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 35 huku nyongeza zikiongezeka hadi karibu pauni 40 milioni.

Post a Comment

0 Comments