Ticker

6/recent/ticker-posts

Robert Lewandowski Arejea Bayern Munich Kuaga rasmi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Robert Lewandowski amerejea Munich kwa ajili ya kuwaaga rasmi wachezaji wenzake wa Bayern baada ya kusajiliwa na Barcelona.

Juhudi za mshambuliaji huyo wa Poland katika Uwanja wa Allianz Arena hazikuishia kwenye kiwango bora kwani aliomba kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Klabu ya Bundesliga hawakutaka kumuuza lakini hatimaye walifika katika makubaliano na  klabu ya Barcelona kwa  mkataba wa miaka 3 na hivyo kuhitimisha uhusiano wake wa miaka 8 na Bayern Munich.

Lewandowski alikuwa miongoni wa wachezaji ya timu ya Barcelona waliosafiri kwenda Marekani kwa ajili ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya kabla ya kuanza kwa msimu wa La Liga.

Mshambulizi huyo alichukua ndege ya kibinafsi hadi Munich mara tu baada ya kutua Barcelona na wachezaji wengine wa timu hiyo, kulingana na gazeti la Ujerumani la Bild.

Taarifa hizo zinasema kuwa meneja wa Barcelona Xavi Hernandez amekupa kikosi hicho siku mbili za mapumziko na Lewandowski anatarajiwa kuzitumia Ujerumani.

Inaarifiwa kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anataka kuwa na sherehe ya kuagwa rasmi kwa njia inayofaa huko Bayern Munich.

Aliendesha  gari  lake hadi Allianz Arena na kupiga picha za kuaga na mataji aliyoshinda Bayern.

Lewandowski alishinda mataji 8 ya Bundesliga katika miaka yake 8 akiwa na Bayern Munich na ndiye mfungaji wa pili bora wa klabu hiyo ya Ujerumani nyuma ya gwiji wa Ujerumani, Gerd Mulller.

Post a Comment

0 Comments