Ticker

6/recent/ticker-posts

Coastal Union yatuma salamu kwa Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KLABU ya Coastal Union imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu NBC 2022/23 baada ya kuichapa KMC bao 1-0 na kuamsha morali kuelekea mchezo wao wa pili dhidi ya Yanga.

Katika Mchezo huo ulipigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha iliichukua timu hiyo dakika 39 kupata bao hilo la ushindi kwa njia ya mkwaju wa penati kupitia kwa mchezaji Moubarack Amza baada ya mlinzi wa KMC FC, Ibrahim Ame kunawa  ndani ya boksi.

Bao hilo lilidumu kwa dakika zote 90 ambapo ushindi huo umeongeza morali kwa Coastal Union FC kuelekea katika mchezo wa pili wa Ligi dhidi ya Yanga ambayo itapigwa Jumamosi hii katika uwanja huo.

Kocha wa Coastal, Juma Mgunda amewapongeza vijana wake kwa kupambana na kuweza kuibuka na ushindi huku akiweka wazi kuwa sasa nguvu zote anaelekeza kwenye mechi ijayo dhidi ya Yanga ambayo ni muhimu kushinda.

Amesema mchezo ulikuwa mgumu wamepata nafasi nyingi lakini wakaweza kutumia moja kama mwalimu anaenda kufanyia kazi sehemu zenye mapungufu hili kuweza kushinda pia mchezo unaofuta.

"Mechi itakuwa ngumu kama mwalimu sasa naenda kukiandaa kikosi kupambana kwa kufanyia kazi mapungufu ambayo nimeona kwenye mechi hii"amesema Mgunda.

Kwa upande wa kocha wa KMC, Thierry Hitimana amesema wamepoteza kutokana na kukosa umakini kwa safu yake ya ushambuliaji ambayo imekosa nafasi nyingi za wazi ambapo sasa anaenda kujipanga kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Polisi Tanzania.

Kikosi cha Coastal kilichoanza kilikuwa na wachezaji Mahamud Mroivili, Nimubona Emery, Miraji Hassan, Khatibu Ally,Lameck Lawi,Betrand Kunfor,Hamadi Majimengi, Mtenje Juma, Maabadi Maabadi, Moubarack Amza na Vicent Abubakary.

Kwa upande wa KMC kikosi kilichoanza kilikuwa na Robert Mapigano, Kelvin Kijili, Isaak Kichwele, Ibrahim Ame, Andrew Chikupe, Baraka Majogoro, George Makanga, Awesu Awesu, Matheo Simon, Ken Mwambungu na Daruwesh Saliboko.

Post a Comment

0 Comments