Ticker

6/recent/ticker-posts

Klabu ya Sporting Lisbon wanataka kumsajili christiano Ronaldo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Mshambuliajiwa Manchester United, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kurejea Sporting Lisbon kwa uhamisho wa bure, klabu ambayo mama yake anataka kumuona akiiwakilisha tena kabla hajafariki.

Sporting Lisbon wameripotiwa kuiambia Manchester United kwamba watakuwa tayari kumsajili Cristiano Ronaldo - lakini kwa uhamisho wa bure tu.

Nyota huyo wa Mashetani Wekundu aliwaichezea klabu hiyo wa Ureno zamani kabla ya kujiunga na United akiwa kijana mwaka 2003.

Mama yake Ronaldo, amekuwa na ndoto ya kumuona mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or akichezea tena Estadio Jose Alvalade, aliwaimwambia kuwa "Mwanangu, kabla sijafa, nataka kukuona ukirudi Sporting."

Na sasa ndoto hiyo inaweza kutimia, kwani gazeti la Independent linadai kwamba Sporting wanataka kumsajili tena mshambulizi wao wa zamani, ambaye anatamani sana kuhama Manchester United msimu huu na kuendelea kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa.

Kufikia sasa, wakala wa Ronaldo Jorge Mendes hajaweza kupata mwenye anayestahili na yuko tayari kulipa mishahara  ya mchezaji huyo ya ziada juu ya ada ya uhamisho.

Klabu ya Sporting wamewasiliana na wakuu wa Old Trafford kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, wakitaka kumsajili kutoka kwa United iwapo watakatisha mkataba wake msimu huu.

Kuanzia msimu huu, mchezaji huyo hajakuwa na ushirikiano poa na wakuu wa klabu ya United baada ya kuonyesha dalili ya kuhama klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments