Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA YATANGAZA TAREHE WIKI YA WANANCHI

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

OFISA  Habari wa Yanga, Haji Manara amebainisha kwamba WIKI ya Mwananchi itaanza rasmi Agosti Mosi mwaka 2022, huku kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2022/23 inatarajiwa kuanza leo Julai 20,2022 Kigamboni.

“Tutafanya kambi yetu Kigamboni ambapo kuna eneo zuri na tulivu kwa ajili ya wachezaji kuweza kupata muda wa kufanya maandalizi ya msimu mpya na ni lazima tufanye maandalizi mazuri.

“Kuhusu Mwananchi Day tutaanza Agosti Mosi na kilele chake itakuwa ni Agosti 6. Itakuwa ni wiki ya kipekee na itakuwa special (maalumu) na bora sana kuliko zote zilizopita.

”Mwisho kabisa tuko tayari kwa maandalizi ya msimu ujao na tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa na tutafanya vizuri,” amesema Manara.


Post a Comment

0 Comments