Ticker

6/recent/ticker-posts

Pep Guardiola azungumzia Neymar kujiunga na Man City

KOCHA Pep Guardiola amekanusha ripoti kwamba Manchester City wamepewa nafasi ya kumsajili Neymar.

Nyota huyo wa Brazil amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka katika mji mkuu wa Ufaransa msimu huu wa majira ya joto, licha ya madai kwamba kocha mpya Christophe Galtier kuwa na mpango nae.

Ripoti za awali ni kwamba PSG walikuwa wanamuhitaji Bernardo Silva, ambaye pia anasakwa na Barcelona, ​​na walikuwa tayari kumtoa Neymar kama sehemu ya dili hilo.


Hata hivyo, Guardiola alikanusha haraka taarifa hizo alipoulizwa kuhusu mpango huo wakati Man City wakiwa ziarani nchini Marekani wakijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi.

"Samahani lakini sio kweli," Guardiola alisema. "Taarifa hizo sio sahihi, Neymar ni mchezaji wa kiwango cha juu sana na taarifa nilizonazo ni mtu mzuri sana. Lakini si kweli kwamba tunamuhitaji."

Man City tayari wamekamilisha usajili wa Erling Haaland, Stefan Ortega na Kalvin Phillips msimu huu wa majira ya joto, huku Julian Alvarez akihusishwa kujiunga na kikosi hicho baada ya uhamisho wake katika msimu wa majira ya baridi kutoka River Plate kukamilika.

Man City wanatarajia kupeleka ofa Brighton kwa ajili ya kumnunua Marc Cucurella mara tu Oleksandr Zinchenko atakapojiunga na Arsenal, lakini wanatakiwa kuandaa kitita kisicho pungua £50m kama ada ya uhamisho kwa beki huyo wa kushoto.

Post a Comment

0 Comments