Ticker

6/recent/ticker-posts

Tyrell Malacia kujiunga Man Utd Muda Wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Tyrell Malacia kujiunga  Man Utd Muda WowoteBEKI wa kushoto wa Feyenoord Tyrell Malacia tayari ametua jijini manchester katika viunga vya Carrington kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Manchester United.

Malacia mwenye miaka 22 alikuwa anatarajia kujiunga na Lyon katika majira haya ya msimu wa joto, lakini dili hilo likaingiliwa kati na Manchester United kutokana na Kocha wa sasa wa United  Erik ten Hag kuvutiwa na beki huyo tangu alipokuwa kuwa nae Ligi kuu ya Uholanzi, hivyo aliwaeleza viongozi wa United kumsajili beki huyo.

Dau la euro milioni 15 limekubaliwa na Feyenoord na Malacia kwa sasa yupo England kukamilisha usajili kujiunga Old Trafford.

Kiungo wa Barcelona Frenkie de Jong ni miongoni mwa wachezaji wanao takiwa na Ten Hag,lakini rais wa barcelona Joan Laporta ameendelea kusisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi, Ingawa timu zote mbili bado zipo katika mazungumzo juu ya uhamisho wa mchezaji huyo.

Christian Eriksen ambaye ni mchezaji huru nae anatakiwa na United na taarifa za uhakika ni kwamba United wameshampa mkataba kiungo huyo, huku wachezaji wawili wa Ajax  Antony na Lisandro Martinez wanafuatiliwa kwa ukaribu na miamba hiyo ya England.

Dau la euro milioni 43 limetumwa Ajax kwajili ya Martinez, Ambae pia anahitajika na Arsenal.

Post a Comment

0 Comments