Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili barani Ulaya: Zinchenko Kwenda Arsenal; Mustakabali wa Ronaldo Man Utd

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Arsenal wapo katika hatua za mwisho kukamilisha Usajili wa mchezaji Oleksandr Zinchenko kutoka Manchester City kwa ada ya uhamisho wa £30m ,Zinchenko atasaini mkataba wa miaka minne Emirates.

Kutokana na hali hiyo, City wanajiandaa kupeleka ofa Brighton kwa ajili ya kumvuta beki wa pembeni, Marc Cucurella kuchukua nafasi ya Mchezaji huyo wa Ukraine anayeondoka na kujiunga na Arsenal.

Licha ya Ronaldo kuomba kuondoka, meneja wa Manchester United Erik ten Hag amedokeza kuwa Cristiano Ronaldo anaweza kuongeza mkataba  Old Trafford.

Atletico Madrid wamethibitisha tena kwamba hawawezi kumnunua Ronaldo huku kukiwa na fununu za mchezaji huyo kutakiwa na miamba hiyo ya Uhispania.

Wakati huo huo, meneja wa Manchester United Erik Ten Hag anafikiria uwezekano wa kubadilishana kiungo wa Milan Ismael Bennacer akimhusisha Donny van de Beek, ambaye bado hajaonyesha kiwango kizuri katika mechi za kujiandaa na msimu mpya.

Beki wa pembeni wa kimataifa wa Ufaransa Jonathan Clauss anakaribia kujiunga na Marseille kutoka Lens, licha ya kutakiwa na Man Utd na Chelsea.

Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga ameibuka kama chaguo namba moja kwa Napoli, ambao wanamtaka Mhispania huyo kwa mkataba wa kudumu. Ross Barkley ni mchezaji mwingine ambaye anatarajiwa kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa majira ya joto, huku Billy Gilmour akitolewa tena kwa mkopo.

Matthijs de Ligt yuko Ujerumani kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Bayern Munich kutoka Juventus.

Licha ya kusajiliwa kwa wachezaji kadhaa,Barcelona bado haijakamilika, Rais Joan Laporta amesema kwamba klabu hiyo bado ina mpango wa kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kuongeza wachezaji.

Real Madrid inajiandaa kuachana na nyota wake baadhi kama Dani Ceballos na Marco Asensio msimu huu wa majira ya joto.Huku Jesus Vallejo, Reinier, Mariano Diaz, Borja Meya na Alvaro Odriozola nao wanaachwa.

Milan wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Club Brugge Charles De Ketelaere, ambaye pia analengwa na Leicester City na Leeds United.

Japhet Tanganga wa Tottenham anatakiwa na Rossoneri, huku miamba hao wa Serie A wakitaka kumchukua beki huyo kwa mkopo.

West Ham wamefufua mazungumzo na mchezaji huru Jesse Lingard na wana uhakika wa kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Amadou Onana kutoka Lille.

The Hammers pia wanapewa nafasi kubwa kumnunua mshambuliaji wa Rennes Martin Terrier, ingawa wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Leeds.

Mshambuliaji Carney Chukwuemeka Inasemekana anataka Mshahara wa £100,000 kwa wiki ili kusalia Aston Villa msimu huu wa majira ya joto, huku kukiwa na tetesi kwamba anatakiwa na vilabu kadhaa maarufu barani Ulaya.

Nottingham Forest wapo katika mipango ya kutaka kumsajili beki wa kushoto Alex Moreno kutoka Real Betis na wanapanga kushindana na Everton kumnunua mshambuliaji wa Burnley, Maxwel cornet.

Post a Comment

0 Comments