Ticker

6/recent/ticker-posts

Mohammed Ouattara kutua Simba Muda Wowote

Klabu ya Al Hilal ya Sudan imethibitisha taarifa za Beki wao Mohammed Ouattara kutoka Ivory Coast  kuondoka klabuni hapo, na kumpa Baraka zote katika maisha yake mapya.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Simba sc ni kwamba Ouattara  kasha kusajiliwa na kasaini mkataba wa miaka miwili.


Ouattara anatajwa kama mrithi wa Pascal Wawa aliyeondoka Simba SC mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kuitumikia klabu hiyo ya Msimbazi kwa misimu minne mfululizo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23, ni pendekezo la Kocha wa sasa wa Simba SC Zoran Maki ambae alifanya nae kazi katika klabu za Wydad Casablanca (Morocco) na Al Hilal (Sudan).

Ouattara anatarajiwa kujiunga na Simba SC wakati wowote ndani ya juma hili, na huenda akaelekea Kambini Ismailia- Misri, moja kwa moja kuungana na wenzake.

Tayari Simba SC imeshakamilisha usajili wa wachezaji watatu wa Kimataifa na kuwatangaza hadharani ambao ni Moses Phiri (Zambia) Victor Akpan (Nigeria) na Augustine Okrah (Ghana).

Wazawa waliosajiliwa klabuni hapo hadi sasa wapo wawili ambao ni Nassoro Kapama na Habib Kyombo.

Post a Comment

0 Comments