Ticker

6/recent/ticker-posts

Robert Lewandowski awaaga wachezaji wenzake wa Bayern Munich kabla ya kuhamia Barcelona

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Robert Lewandowski awaaga wachezaji wenzake wa Bayern Munich kabla ya kuhamia Barcelona

Robert Lewandowski amethibitisha kuwa amewaaga wachezaji wenzake wa Bayern Munich huku akikaribia kujiunga na Barcelona.

Lewandowski hakuficha nia yake ya kutaka kujiunga na Barca katika msimu huu wa majira ya joto, baada ya kuzungumza hadharani mara kadhaa akiwataka Bayern wamruhusu aondoke zake .

Uhamisho huo ulitiliwa shaka kwa muda kutokana na matatizo ya kifedha ya Barca lakini baada ya klabu hiyo kutumia 'njia mbadala' katika kufufua uchumi wao hivi karibuni, uhamisho huo sasa unapaswa kukamilika haraka.

Barcelona wanataka kukamilisha usajili huo mwishoni mwa juma na wamekubali kulipa kiasi cha €50m kama ada ya uhamisho kwa mchezaji huyo kutoka ​​Bayern.

Lewandowski alithibitisha kwamba atakuwa kwenye harakati za kuondoka baada ya kukamilisha mazoezi yake ya mwisho akiwa na Bayern.

"Nitarudi  kuwaaga wafanyakazi wote ipasavyo. Sikuwa na muda mwingi wa kujiandaa kwa hilo sasa," mshambuliaji huyo aliambia Sky Sports Germany.

"Miaka hii minane ilikuwa maalum na uwezi sahau hilo. Nilikuwa na wakati mzuri nikiwa Munich. Nitapanda ndege hivi karibuni, lakini baada ya kambi ya mazoezi nitarejea tena kuaga vizuri na kukamilisha vitu vichache.

"Nimewaaga wachezaji wenzangu uwanjani leo sikuwa na wasiwasi kuhusu kupata majeraha katika mazoezi. Kwani chochote kinaweza kutokea nikiwa nyumbani. Nilitaka kujiweka sawa kwa kufanya mazoezi tena na vijana wangu."

Lewandowski anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Barcelona katika kipindi hiki cha usajili baada ya Franck Kessie, Andreas Christensen na Raphinha. Ousmane Dembele amekubali kusaini kandarasi mpya baada ya mkataba wake wa awali kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.

Post a Comment

0 Comments