Ticker

6/recent/ticker-posts

Robert Lewandowski awasili Uhispania kujiunga na Barcelona

 Robert Lewandowski awasili Uhispania kujiunga na Barcelona


Robert Lewandowski amewasili nchini Uhispania kufanyiwa vipimo vya Afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Barcelona ambao ulikuwa unasubiriwa kwa muda mrefu.


Bayern Munich wamethibitisha kuwa wamefikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji huyo wa Poland mapema Jumamosi, nao Barcelona wakathibitisha hilo muda chache baadaye.


"FC Barcelona na Bayern Munich wamefikia makubaliano mapema ya uhamisho wa Robert Lewandowski, Ikisubiri vipimo vya Afya vya mchezaji huyo na kusainiwa kwa mikataba," ilisema taarifa ya Blaugrana(Barca).


Uhamisho huo umefika mahara pazuri baada ya Lewandowski kuwasili Mallorca leo jioni kabla ya kufanyiwa vipimo vya Afya.


Pande zote mbili zimekubaliana Ada ya Uhamisho takriban €50m, na kumaliza mazungumzo ya muda mrefu ambayo yalionekana kutaka kusambaratika mapema hapo mwanzoni.


Chelsea na Manchester United wote walikuwa wameomba kufahamishwa kuhusu mustakabali wa Lewandowski, lakini mchezaji huyo kwa muda mrefu amekuwa akiweka bayana kwamba anapenda kuhamia Camp Nou msimu huu wa majira ya joto, na sasa anakaribia kutimiza ndoto yake.


Post a Comment

0 Comments